YANGA wameendeleza mwendo ambao siyo mzuri katika michuano ya kimataifa baada ya kuruhusu kupata kichapo kutoka kwa Gor Mahia cha mabao 3-2 kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga wameshacheza michezo minne hadi sasa kwenye Kundi D ambalo lina timu nyingine ambazo ni USM Algers ya Algeria na Rayon Sports ya Rwanda, lakini hawajapata ushindi kwenye mchezo hata mmoja.
Matokeo ya mchezo wa jana yanamaanisha kuwa sasa Yanga wamebakiza michezo miwili tu kwenye kundi lao na hawana matumaini ya kufuzu. Katika michezo miwili ambayo Yanga wamekutana na Gor Mahia hivi karibuni, wamefungwa jumla ya mabao saba, baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 4-0 jijini Nairobi.
Katika mchezo wa jana, kipa wa Yanga, Youth Rostand alifanya makosa kadhaa ambayo yalichangia mabao mawili ya mwanzo ya Gor Mahia.
Rostand alifanya kosa katika sekunde ya 35 tangu kuanzia kwa mchezo hu ambapo aliucheza mpira vibaya uliopigwa kichwa na George Ogutu na kujaa wavuni.
Hata hivyo, aliendelea kufanya makosa ya mara kwa mara ambapo dakika ya 41 kipa huyo aliudaka mpira akaurusha vibaya kabla haujaguswa na mchezaji mwingine akaudaka tena, mwamuzi akaamuru kuwa ni faulo ambapo Jacques Tuisenge aliifungia timu hiyo bao la pili.
Dakika ya 55, Deus Kaseke, ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe na Yanga, hivi karibuni aliifungia timu yake bao moja baada ya kipa wa Gor Mahia, Boniface Oluoch kuutema mpira.
Hata hivyo, matumaini ya Yanga hayakudumu kwani dakika ya 64, Gor Mahia walifunga bao la tatu kupitia kwa Haron Shakava baada ya mabeki wa Yanga kufanya uzembe. Dakika ya 75, Yanga walimtoa Rostand na nafasi yake kuchukuliwa Beno Kakolanya ambapo wakati anatoka mashabiki walikuwa wakimzomea.
Dakika tano baadaye Raphael Daudi aliifungia timu hiyo bao la pili baada ya kipa kushindwa kukoa shuti lililopigwa na Ibrahim Ajibu. Hata hivyo, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera hakuonekana kwenye mchezo huo ambapo Noel Mwandila ndiye alikuwa anatoa maelekezo kwenye benchi.
About Me
Popular Posts
-
Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa hana kinyongo na kutoa ba...
-
Leo June 19, 2018 Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amemtabiria Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa kuchukua jimbo l...
-
Leo June 20, 2018 nakusogezea stori kumhusu Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ambaye ameongezeka katika list ya wavumbuzi wa magari ya nisha...
-
SERIKALI imepeleka sh. bilioni 2.6 katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kugharamia uboreshaji wa vituo vya afya ili kuimaris...
-
Wikiendi hii imekuwa ni ya nenda kwa usalama katika mitandao ya kijamii kutokana na habari kubwa kabisa ya mh rais kuteuwa viongozi mbalim...
-
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ku...
-
Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani alimaarufu kama 'Mzee Majuto' amefunguka na kuweka wazi ugonjwa ambao unamsumbua kw...
-
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kuhusika na t...

No comments:
Post a Comment