Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi
Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
kuihoji juu ya tuhuma zinazowakabili.
Benki hiyo inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
“Leo tumewaita na tutakutana nao. Baada ya kukutana nao
taarifa tutaiwasilisha kwa Spika kama alivyotuagiza," amesema mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka ambaye
pia ni mbunge wa Same Mashariki (Chadema)
Tuhuma kuhusu BoT ziliibuliwa na mbunge wa Ulanga (CCM),
Goodluck Mlinga Juni 4, 2018 bungeni
katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2018/19.
Mlinga amesema BoT inatumia Sh12bilioni kwa mwaka badala ya
Sh1bilioni kugharamia matibabu ya watumishi wake.

No comments:
Post a Comment