Coastal Union Yafunguka Kuhusu Kumsajili AliKiba
Uongozi wa klabu ya Coastal Union ‘Wagosi wa kaya’ umefunguka na kuthibitisha kuwa katika mazungumzo na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ili waingie naye mkataba rasmi kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.
Hafidh Kido ambaye ni Afisa habari wa klabu hiyo amesema kuwa tetesi hizo kwa kiasi kidogo zina ukweli japo mambo bado hayajakaa sawa kiasi cha kuweza kutangazwa huku akikiri uwezo wa mchezaji huyo.
“Alikiba nadhani nyie wenyewe mnamuona uwezo wake sio wa kiwango cha juu ni kwasababu tu hana mazoezi ya mara kwa mara na kucheza mechi, lakini Alikiba huwezi ukabeza kiwango chake hata siku moja“. Amesema Hafidh.
Kigezo kikubwa ambacho wanajadiliana na Alikiba ni jinsi gani mkataba wao utakavyokuwa kutokana na msaniii huyo kujihusisha kwa kiasi kikubwa katika kazi yake nyingine ya muziki.
Pia Hafidh amezungumzia kuhusu sababu ya wao kutotangaza usajili wowote mpaka sasa huku dirisha la usajili likielekea ukingoni wiki hii.
“ Usajili wetu bado, kocha anaendelea na uchambuzi wake na orodha ikishakamilika tutatangaza rasmi ili kuepuka migongano ya mikataba ya wachezaji na timu zingine, kwahiyo dirisha likikaribia kufungwa ndipo tutatangaza rasmi nani tunaye na nani hatunaye".
Coastal Union imepanda daraja msimu uliopita na sasa iko katika maandalizi rasmi Jijini Dar es Salaam ya msimu mpya wa ligi ambao unatarajia kutimua vumbi kuanzia Agosti 22 .
About Me
Popular Posts
-
Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa hana kinyongo na kutoa ba...
-
Leo June 19, 2018 Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amemtabiria Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa kuchukua jimbo l...
-
Leo June 20, 2018 nakusogezea stori kumhusu Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ambaye ameongezeka katika list ya wavumbuzi wa magari ya nisha...
-
SERIKALI imepeleka sh. bilioni 2.6 katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kugharamia uboreshaji wa vituo vya afya ili kuimaris...
-
Wikiendi hii imekuwa ni ya nenda kwa usalama katika mitandao ya kijamii kutokana na habari kubwa kabisa ya mh rais kuteuwa viongozi mbalim...
-
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ku...
-
Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani alimaarufu kama 'Mzee Majuto' amefunguka na kuweka wazi ugonjwa ambao unamsumbua kw...
-
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kuhusika na t...
No comments:
Post a Comment