Jaji
Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani amemzungumzia Jaji Robert Kisanga kuwa mtu
aliyebobea katika taaluma na hakuwahi kujihusisha na rushwa.
Amesema
hayo leo Alhamisi Januari 25,2018 Oysterbay jijini Dar es Salaam alikokwenda
kuhani msiba wa Jaji Kisanga (85).
Jaji
Ramadhani amesema hakuna hata siku moja aliwahi kusikia malalamiko dhidi ya
Jaji Kisanga kutokana na uadilifu wake.
"Mimi
ni miongoni kwa watu waliopitia kwenye mikono yake, yeye ndiye aliyenifundisha
masuala ya Mahakama ya Rufaa," amesema.
Amesema,
“Alikuwa mahiri kwenye kazi na kama uko naye kwenye kesi ni muhimu usome sana
kwa sababu alikuwa anasoma na kila jambo alilichimba kwa undani."
Jaji
Ramadhani amesema, "Naweza kusema ni miongoni mwa majaji waadilifu, kwake
rushwa ilikuwa mwiko, hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo ndiyo sababu
sikuwahi kusikia malalamiko dhidi yake."
Amesema
majaji wanatakiwa kujifunza tabia hiyo kutoka kwa Jaji Kisanga.
"Majaji
wanapaswa kutambua kuwa hakuna kitu kibaya kama kuuza utu wa mtu, mwenzetu
Kisanga alizingatia mno sheria na hata mawakili waliokuwa wanapangiwa kesi
kwake walikuwa wanajipanga," amesema.
Jaji
Kisanga alifariki dunia Jumanne Januari 23,2018 katika Hospitali ya Regency
jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani.
No comments:
Post a Comment