Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ruby, amewatolea povu watanzania kutokana na tabia zao za kuongea sana na kuwakatisha watu tamaa, badala ya kuwatia moyo na kuwafariji, baada ya post yake instagram.






 Ruby amesema amewavumilia watanzania kwa tabia zao za kutazama vitu kwa mtazamo hasi na kuvunjana moyo, lakini ameona ni bora awaleze kwani sio jambo zuri kwa mtu yeyote.
“Watanzania tuache midomo tuna mdomo sana, hiyo post haimuhusu mtu yeyote na wala sipo desperate isipokuwa nimehitaji kufunguka kwa sababu kila siku nachoshwa na tabia za watanzania, yani sizipendi sikubali, kuna muda unajiuliza hii ni nchi yangu!!? mbona kama niko sehemu tofauti sana”, amesema Ruby.
Hivi karibuni Ruby amekuwa akishutumiwa kushuka kimuziki baada ya kukorofishana na uongozi wake wa awali, huku wakidai nafasi yake kuchukuliwa na Nandy ambaye anafanya vizuri kwa sasa licha ya kujaribu kurudi kwenye game.

godfrey

No comments:

Post a Comment

Instagram